MABORESHO MAKUBWA YA HUDUMA NDANI YA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA KAG
Posted on: February 4th, 2026Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba (BRRH) Kagera Museleta Nyakiroto, amesema uwepo wa huduma za kibingwa pamoja na madaktari bingwa katika hospitali hiyo umeleta manufaa makubwa kwa wananchi wa mkoa wa Kagera, ikiwemo kupunguza gharama za kusafiri kwenda mikoani kwa ajili ya matibabu.
Dkt. Nyakiroto ameyasema hayo katika kipindi cha Nuru ya Asubuhi kinachorushwa na Muleba FM, ambapo ameeleza kuwa utoaji wa huduma za kibingwa kwa wakati umeongeza ufanisi mkubwa katika matibabu ya wagonjwa.
Amefafanua kuwa kwa sasa hospitali hiyo ina jumla ya madaktari bingwa 11 wakiwemo wa magonjwa ya watoto, akina mama na uzazi, Macho, Masikio, Pua na Koo, Upasuaji, Kinywa na Meno, Magonjwa ya Ndani hali iliyosaidia wananchi kupata huduma karibu na walipo.
Dkt. Nyakiroto ameongeza kuwa hospitali hiyo pia inatoa huduma za vipimo na uchunguzi wa kisasa ikiwemo huduma ya CT Scan, Ultra Sound na X-Ray, ambazo zimeongeza ufanisi katika utendaji kazi na kuboresha utoaji wa huduma za afya.
Kwa upande mwingine, amewahimiza wananchi wa Mkoa wa Kagera kuwahi kupata huduma za matibabu pindi wanapohisi dalili za ugonjwa, ili kuepuka kufika hospitalini hali ikiwa imekuwa mbaya zaidi.
Aidha, ameongeza kuwa, Serikali imeendelea kuwekeza katika miundombinu ikiwemo uijenzi wa jingo la Wagonjwa Mahututi (ICI), Jengo la Dharura (EMD) pamoja na jingo la CT- SCAN huku akisisitiza kuwa wapo katika hatua za Mwisho kuanza ujenzi wa jingo la Mama na Mtoto lenye ulefu wa orofa nne.





