WANANCHI WA KYERWA WAHIMIZWA KUJITOKEZA KAMBI MAALUM YA MATIBABU YA MACHO
Posted on: December 1st, 2025Wananchi wa Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, wameendelea kuhamasishwa kujitokeza kwa wingi katika kambi maalum ya uchunguzi na matibabu ya afya ya macho inayoendeshwa katika Kituo cha Afya Nkwenda kuanzia leo tarehe 01 hadi 05 Desemba 2025.Rai hiyo imetolewa na Mganga Mfawidhi wa kituo Dkt. Nathaniel Ngeta ametoa akiwasisitiza wakazi wa maeneo mbalimbali ya Kyerwa kuitumia fursa hiyo adimu ya kupima macho na kupata matibabu kutoka kwa timu ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa,Bukoba.
Amesema kuwa, huduma hizo ni muhimu katika kusaidia jamii kugundua mapema matatizo ya macho na kupata tiba stahiki.
Akitoa taarifa ya mwenendo wa kambi hiyo kwa siku ya kwanza, Mganga Mfawidhi ameeleza kuwa jumla ya wananchi 160 wamehudumiwa leo, ikiwa ni ishara ya mwitikio mzuri kutoka kwa wananchi.
Ameongeza kuwa, huduma ya kumuona daktari ni bure kabisa, huku wananchi wanaohitaji dawa, miwani au upasuaji wakichangia kiasi kidogo tu cha gharama.
Kwa upande wake, Daktari Bingwa wa Macho kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Bukoba, Dkt. Daniel Mashamba, amesema kuwa huduma zinazotolewa zinajumuisha uchunguzi wa kina wa macho, utoaji wa dawa, upimaji na utoaji wa miwani, pamoja na upasuaji kwa wagonjwa wanaogundulika kuwa na tatizo la mtoto wa jicho (cataract).
Kambi hiyo ya matibabu imeratibiwa naHospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba kwa kushirikiana na shirika la KCCO, chini ya udhamini wa Australia Aids, ikiwa na lengo la kuboresha upatikanaji wa huduma za macho kwa jamii za maeneo ya vijijini.
Wananchi wa Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, wameendelea kuhamasishwa kujitokeza kwa wingi katika kambi maalum ya uchunguzi na matibabu ya afya ya macho inayoendeshwa katika Kituo cha Afya Nkwenda kuanzia leo tarehe 01 hadi 05 Desemba 2025.
Rai hiyo imetolewa na Mganga Mfawidhi wa kituo Dkt. Nathaniel Ngeta ametoa akiwasisitiza wakazi wa maeneo mbalimbali ya Kyerwa kuitumia fursa hiyo adimu ya kupima macho na kupata matibabu kutoka kwa timu ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa,Bukoba.