Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Bukoba
(Government Hospital)

BUKOBA_RRH YAANZA RASMI KUTOA HUDUMA YA KLINIKI UPASUAJI NA MATIBABU KWA WATOTO WENYE VICHWA KUJAA MAJI ISIVYO KAWAIDA NA MGONGO WAZI.

Posted on: July 15th, 2024

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba (BUKOBA_RRH)  imeanza rasmi kutoa Huduma ya matibabu, upasuaji na kliniki kwa watoto wenye matatizo ya kichwa kujaa maji isivyo kawaida na mgongo wazi wanaoletwa hospitali hapa baada ya wataalamu kutoka BUKOBA_RRH kuhitimisha mafunzo kwa vindendo jinsi ya kuwahudumia  watoto hao.


Akitoa taarifa ya kuanzishwa kwa huduma hiyo, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba Dr. Museleta Nyakiroto amesema kuwa, mwezi Aprili 2024 hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba ilipokea Madaktari Bingwa wa Upasuaji Mishipa ya Fahamu (Ubongo na Mgongo) pamoja na wataalamu wa Usingizi kutoka Hospitali ya Kanda Bugando wakiwa na lengo la Kutoa huduma ya mabibabu na upasuaji BURE kwa watoto wenye matatizo ya Mgongo wazi na Kichwa kujaa Maji isivyo kawaida pamoja na kuwajengea uwezo wataalamu wetu wa BUKOBA_RRH jinsi ya kuwahudumia na  kuwafanyia upasuaji watoto wenye matatizo hayo.


“Lengo la wataalamu hawa kuja hapa kiukweli limetimia kwani baada ya kufika hapa waliweza kujengea uwezo wataalamu wetu kwa njia ya nadaharia na vitendo ambapo kupia wataalamu hao jumla ya watoto 83 weny tatizo la mgongo wazi na vichwa kujaa maji 83 walionwa na madaktari hao kwa kushirikiana na wa madaktari na wataalamu wetu na kati yao  watoto 31 wameweza kufanyiwa upasuaji, kutokana na juhudi hizo wataalamu kutoka Bugando wamejiridhisha kuwa wataalamu wetu wameiva na wanaweza kuendelea kutoa huduma hii kwa ustadi mkubwa na sasa tunaanza rasmi kutoa huduma  hii hapa hospitalini kwetu”


Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Upasuaji Mishipa ya Fahamu (ubongo na mgongo) kutoka Hospitali ya Kanda ya Bugando  Dr.Gerald Mayaya amesema kuwa, wataalamu hao wakishirikiana na shirika la MWADETA wameamua kuwajengea uwezo Madaktari na wataalamu kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba ili kupunguza au kuondoa kabisa  rufaa za watoto wenye matatazo ya Vichwa kujaa Maji na Mgongo ambazo walikuwa walizipokea kutoka Mkoani Kagera