Watumishi wa Afya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba (BRRH) wakipatiwa elimu
Posted on: September 1st, 2023Watumishi wa Afya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba (BRRH) wakipatiwa elimu namna ya utunzaji wa Vifaa Tiba hospitalini katika kikao cha ‘Continous Medical Education’ (CME) kilichofanyika leo Septemba 01, mwaka huu.
Elimu hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitengo cha Vifaa Tiba Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba (BRRH), Mhandisi David John Matewele kwa watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba wakiongozwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba Dakt. Museleta Nyakiroto.
Aidha, watumishi wameelekezwa na kukumbushwa mbinu bora za utunzaji wa Vifaa Tiba hospitalini ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.