Historia ya Hospitali
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba Miongoni mwa Hospitali Kongwe Hapa Tanzania. Hospitali hii ilianzishwa Mwaka 1923 ikiwa kama kambi ya Jeshi la koloni la Kijerumani, kwa baada ilipandishwa hadhi na kubadilishwa kuwa Zahanati hatimaye kuwa Hospitali. Tarehe 12 Novemba, 2010 Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kupitia Gazeti lake namba 828 ilitangaza kuipandisha hadhi Hospitali hii na kuwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa. Hospitali inapatikana katikati ya Viunga vya Manspaa ya Bukoba Mkoani Kagera Kaskazini Magharibi mwa tanzania ikiwa na umbali wa kilometa 1450 kutoka Dae es Salaam na Kilometa 450 kutoka Mwanza.
Idadi ya Watu na Makazi.
Hospitali hutoa huduma mkoani Kagera kwa Halmshauri Nane (8) zifuatazo:- Halmshauri ya Wilaya ya Bukoba Vijinini, Halmshauri ya Wilaya ya Bukoba Manispa, Halmshauri ya Wilaya ya Karagwe, Halmshauri ya Wilaya ya Muleba, Halmshauri ya Wilaya ya Ngara na Halmshauri ya Wilaya ya Biharamulo. Hivyo hupokea rufaa kutoka vituo vya kutolea afya 304 ikiwa ni Hospitali 13, Vituo vya Afya 31 na Zahanati 260 ikiwa idadi ya wakazi ni 2,913,093 [Sensa 2012]. Hospitali ina jumla ya vitanda 308 na Wastani wa Wagonjwa wa nje 515 kwa siku na wagonjwa wa kulazwa 34 kwa siku.