Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Bukoba
(Government Hospital)

DR. RUTABASIBWA KUTOKA MUHIMBILI AFIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA, BUKOBA NA KUPONGEZA UTENDAJIKAZI WA TIMU YA MADAKTARI IDARA YA UPASUAJI BRRH.

Posted on: February 10th, 2024

Daktari Bingwa Mbobezi wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dr. Nicephorerus Rutabasibwa ameitembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba (BRRH) na kutoa pongezi nyingi kwa Madaktari wa Idara ya Upasuaji BRRH jinsi wavyoshirikiana katika kuokoa maisha ya wananchi wanaofika BRRH kupata huduma ya upasuaji ikiwa ni pamoja na upasuaji wa fuvu la kichwa.

Dr. Rutabasibwa ametoa pongezi hizo wakati akiwasilisha mada katika CME iliyofanyika katika ukumbi wa Ukumbi wa BRRH na kuhudhuriwa na watumbishi mbalimbali kutoka Hospitali ya Rufa ya Mkoa, Bukoba ambapo alisema kuwa, baada ya kufika BRRH ameweza kuzunguka na kukutana na wagonjwa ambao wamefanyiwa upasuaji hususani upasuaji wa kufungua fuvu na wagonjwa hao wanaendelea vizuri.

“Kiukweli nampongeza Dr. Nyakiroto ambaye ndiye Mkuu wa Idara ya Upasuaji pamoja na timu yake, baada ya kufika hapa Hosiptali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba nimeweza kuwaona wagonjwa mbalimbali ambao kwa bahati nzuri wameishaanza kufanyiwa upasuaji, Timu ya Madaktari imeishaanza kufanya upasuaji wa kufungua fuvu, na mimi nikaona kwakuwa nipo hapa BRRH niweze kushirikiana nao katika kuwaona wagonjwa na kushauriana ili tuweze kuona ni mgonjwa gani ambaye anahitaji kufanyiwa upasuaji na baada ya upasuaji tumfanyie nini”

Ameongeza kuwa, baada ya kufika BRRH aliweza pia kutembelea sehemu mbalimbali za Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba na kujionea miundombiniu mizuri na mitambo ya kisasa ikiwa ni pamoja na uwepo wa ICU ya kisasa na mashine mpya ya CT-SCAN, yote kwa pamoja inawawezesha madaktari wa upasuaji kuendelea kufanya kazi yao vizuri huku akiahidi kuwa, atakuwa anaitembeleana BRRH mara kwa mara ili kuendelea kubadilishana uzoefu na madaktari wa BRRH.

Kwaupande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba Dr. Museleta Nyakiroto amempongeza Dr. Nicephorerus Rutabasibwa kwa kuitembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba kwa na kubadilishana mawazo na Madaktari pamoja na watumishi wa Afya.