KAMBI YA MAALUMU YA MATIBABU YA UPASUAJI WA FISTULA YAANZA RASMI KATIKA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA, BUKOBA
Posted on: May 19th, 2024Kambi ya siku tano ya matibabu ya upasuaji wa Fistula na msamba imeanza rasmi siku ya leo tarehe 20.05.2024 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba.
Kambi hiyo inaendeshwa na timu ya Madaktari kutoka Chama cha Madaktari wa Upasuaji wa Fistula Tanzania (AOFST) Kwakushirikiana na Wizara ya Afya, Shirika la Fistula Foundation pamoja na Wataalam kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba.
Kupitia kambi hii akina mama wenye ugonjwa huu wamepatiwa matibabu bure na kulipiwa gharama za usafiri.