MGANGA MFAWIDHI HOSPITALI YA BUKOBA AWAOMBA WANANCHI WA MKOA WA KAGERA KUSHIRIKIANA BRRH KATIKA UELIMISHAJI WA JAMII JUU YA UGONJWA WA SELIMUNDU
Posted on: September 12th, 2023Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba (BRRH), anapenda kuwataarifu wananchi wote wa Mkoa wa Kagera kuwa, Mwezi huu wa Septemba ni mwezi wa uelimishaji wa jamii juu ya ugonjwa wa Selimundu (SICKLE CELL DISEASE).
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba kwa kushirikiana na Wizara ya Afya wanaungana na Dunia nzima katika kuadhimisha mwezi huu wa uelimishaji jamii na uchunguzi wa awali juu ya ugonjwa wa Selimundu.
Hivyo basi, wananchi wote mnatangaziwa kuwa kutakuwepo na zoezi la uelimishaji wa jamii juu ya ugonjwa wa Selimundu kwa kufanya uchunguzi wa awali kwa watoto wote watakaozaliwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba mwezi huu pamoja na kutoa ushauri kwa wananchi wanaotarajia kufunga ndoa.
Aidha, Kwa watoto wote watakaozaliwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba katika kipindi hiki cha mwezi Septemba watapatiwa huduma hii bure. Wote mnakaribishwa kwa huduma hii.