Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Bukoba
(Government Hospital)

RC MWASSA AWASIHI WANANCHI WA MKOA WA KAGERA KUENDELEA KUFIKA BRRH KWA AJILI YA KUPIMA NA KUFANYIWA UCHUNGUZI WA MAGONJWA YA MOYO

Posted on: March 20th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Kagera Hajati Fatma Mwassa amewasihi wananchi wa Mkoa wa Kagera kuendelea kuchangamkia fursa ya kufika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba (BRRH) kwa ajili ya kupima na kuchunguza magonjwa ya moyo kutokana na uwepo wa kambi maalumu ya uchunguzi wa magonjwa ya moyo inayoendeshwa na madaktari bingwa wa magojwa ya moyo kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.

Ameyasema hayo leo wakati akifungua kambi hiyo ya kibingwa inayoanza kutolewa kuanzia Machi 18 na inategemea kuhitimishwa Machi 22 mwaka huu, amabapo wananchi wa Mkoa wa Kagera na mikoa ya jirani waendelea kupatiwa huduma za kibingwa ikiwa ni pamoja na kipimo cha kuangalia moyo unavyofanya kazi, kipimo cha kuangalia mfumo wa umeme wa moyo, kutoa ushauri wa lishe bora pamoja na kupima utizo na urefu.

“Tuna kila sababu ya kuendelea kumshukuru  rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa aliyoifanya na anayoendelea kuifanya katika kuboresga sekta ya Afya, serikali ya awamu ya sita imefanikiwa kuleta mashine mpya na za kisasa zinazotusaidia wananchi kupata matibabu katika Hospitali yetu ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba vipimo hivi vimewasaidia pia wataalamu wa JKCI kutoa huduza za uchunguzi kwa urahisi kwani Vifaa wamevikuta hapa, hivyo nitoe rai kwa wananchi wa mkoa wa kagera kuendelea kufika hapa hospitali kufanyiwa vipimo vya magonjwa ya moyo na kujua hali zao”

Aidha, ameupongeza uongozi pamoja na madakatari bingwa kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete kwa kufika wa Kagera ili kutoa huduma za vipimo mbalimbali vya magonjwa ya moyo huku akiwasihi kuendelea kuutembelea mkoa huu ili kuwasaidia wananchi kupata huduma hizi karibu.

Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba Dr. Museleta Nyakiroto amemshuku Mkuu wa Mkoa wa KageraHajati Fatma Mwassa kwa kufika na kufungua rasmi utoaji wa huduma za kibingwa huku akisisitiza  kuwa lengo ya kambi hii ni kusogeza huduma za kibingwa na ubingwa  bobezi karibu na wananchi ili kuwapunguzia adha ya kufuata huduma hizo katika mikoa ya mbali ukiwemo Mkoa wa Dar Es Salaam na Mwanza.

Aidha, ameongeza kuwa katika kambi hii wananchi wanapata huduma zote za vipimo ya mayo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba huku akisisitiza kuwa mnamo mwezi Aprili 08, 2024 wanategemea kuwa kambi maalumu nyingine ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Kanda ya Bugando watakaokuja kutoa huduma kwa Watoto wenye matatizo ya vichwa maji na wanaozaliwa mgongo wazi.

Akitoa Taarifa fupi kwa niaba ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Dr. Yona Gandye ameushukuru uongozi wa Mkoa Kagera, Hospitali ya Rufaa ya  Mkoa, Bukoba na wananchi  kwa ujumla kwa mapokeo mzuri na kujitokeza kwa wingi kufanya vipimo na uchunguzi wa magonjwa ya moyo.

Sambamba na hilo akisisitiza kuwa Taasisi ya JKCI imekuwa na utaratibu wa kuwafauata wananchi walipo na kutoa huduma za za Tiba mkoba ya matibabu ya kibingwa ya moyo zijulikanazo kwa jina la Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan Outreach Service inayowawezesha kuwafikia wananchi wengi kwa ajili ya kuwapatia matibabu ya moyo kwa wakati.