Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Bukoba
(Government Hospital)

WATUMISHI WA AFYA BRRH WAMEENDELEZA UTAMADUNI WAO WA KUPIMA AFYA ZAO

Posted on: November 15th, 2023

Watumishi wa Afya kutoka Idara na Vitengo tofauti tofauti Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba (BRRH) wamejitokeza kwa wingi kupima afya ili kuweza kutambua afya zao.

Watumishi hao wamejitokeza kupima zao baada ya Kitengo cha Magonjwa ya Ndani kwa kushirikiana na Kliniki Kufua Kikuu (T.B) Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba kutoa huduma ya uchunguzi wa kifua kikuu bure kwa watumishi wote kwa wa BRRH kuanzia siku ya Jumatatu Novemba 13, 2023 hadi leo siku ya Jumatano Novemba 15.2023.


Sambamba na huduma ya uchunguzi watumishi hao wamekumbushwa kuwa,  dalili za kifua kikuu za kifua kikuu kuwa ni pamoja na kutokwa jasho jingi nyakati za usiku, kikohozi kwa wiki au Zaidi, kukohoa makohozi yaliyochangamana na damu, kupungua uzito na homa.


Aidha, wameelezwa njia za kuzuia maambukizi ya vimelea vya kifua kikuu kuwa ni pamoja na kufunika mdomo na pua kwa kutumia kitambaa laini wakati wa kukohoa, kufungua madirisha kuruhusu hewasafi na mwanga wa jua, kuwahi katika kituo cha kutolea huduma ili kupata huduma za vipimo na   matibabu.