Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Bukoba
(Government Hospital)

WATUMISHI WA AFYA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA, BUKOBA WAPATIWA MAFUNZO YA LUGHA YA ALAMA.

Posted on: October 26th, 2023


WATUMISHI wa Afya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba (BRRH) wamepatiwa mafunzo ya lugha ya alama kutoka kwa wataalam wa lugha ya alama BRRH baada ya kupatia mafunzo ya lugha ya alama yaliyotolewa na Wizara ya Afya.

Mafunzo hayo yametolewa leo Oktoba 27, 2023 kwenye kikao cha Mfunzo Kazini (CME) yaliyofanyika katika ukumbi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo watumishi wa afya  BRRH ili kurahisisha  mawasiliano baina ya watoa huduma wa BRRH na wagonjwa wenye ulemavu wa usikivu wanatembelea  Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba kwa ajili ya  kupata huduma za afya.

Wataalamu hao wa lugha ya Alama ambao ni Aisha Dallu ambaye ni Afisa Ustawi BRRH, Dr. Carlos Christian pamoja na Jovitha Jonathan ambaye ni mwenyekiti wa chama cha viziwi Mkoa wa Kagera wamefundisha mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na alama za alfabeti, alama za namba, alama za wakati pamoja na alama za salamu.